August 13, 2026

Swahili Orthodox Chants & Teachings

Ili kwa nia moja tuungame: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Apolitikio na Maisha ya Mtk. Makarios wa Misri



Mtk. Makari(os) Mkuu alikuwa mwanafunzi wa Mtk. Antoni(os) Mkuu. Alizaliwa mwaka wa 301 huko Misri. Alijiunga na utawa miakani ya ujana wake na huko ndiko alikokutana na Mtk. Antoni(os) na kujiunga naye. Walizoea kumwita “Mzee mtoto” kwa sababu ya umri wake mdogo uliojawa na hekima nyingi na uadilifu wa maisha. Mtk. Makari(os) alikuwa anajulikana kama mwenye kujawa na Roho Mtakatifu na mwenye mienendo isiyo ya kawaida machoni pa watu. Alijiepusha sana na ustaarabu wa kidunia na badala yake kufuata Roho wa Mungu. Hapo mwakani 331, watawa wengi walijiunga naye na kuunda jamii ya utawa chini ya uongozi wake. MAKARI(OS) ATAWAZWA KUWA KASISI Hata ingawa yeye mwenyewe alijiona kuwa mwenye dhambi na asiyestahili kuwa kwenye ofisi takatifu ya ukasisi, hatimaye alitawazwa kuwa kasisi. Bila ya mashauriano yoyote, alihamishiwa kwenye kisiwa kidogo cha Nile na Mfalme Valeni aliyekuwa mfuasi wa mafunzo potovu ya Aria. Vipaji vyake vya kuhubiri na kuponya hata hivyo, vilifuatana naye na akaweza kufanya wengi kuwa Wakristo…..

source