August 13, 2026

Swahili Orthodox Chants & Teachings

Ili kwa nia moja tuungame: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Apolitikio ya Mtakatifu Yohana Krisostomu (Nov 13)



NEEMA ing’aayo toka kinywani mwako kama taa imeuangazia ulimwengu, imeifichulia dunia hazina ambazo mali haiwezi kununua, na kutuonyesha kimo cha unyenyekevu, sawa na kutuelekeza kwa maneno yako, Ee Baba Yohana Krisostomu1, pia ututetee kwa Neno, Kristo Bwana wetu, ili nafsi zetu ziokolewe.

1Krisostomu – Mwenye kinywa cha dhahabu; yaani, azungumzaye maneno ya busara

source