August 13, 2026

Swahili Orthodox Chants & Teachings

Ili kwa nia moja tuungame: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Apolitikio ya Mtk. Yohana Krisostomu (Novemba 13)



NEEMA ing’aayo toka kinywani mwako kama taa imeuangazia ulimwengu, imeifichulia dunia hazina ambazo mali haiwezi kununua, na kutuonyesha kimo cha unyenyekevu, sawa na kutuelekeza kwa maneno yako, Ee Baba Yohana Krisostomu, pia ututetee kwa Neno, Kristo Bwana wetu, ili nafsi zetu ziokolewe.

source