August 13, 2026

Swahili Orthodox Chants & Teachings

Ili kwa nia moja tuungame: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

NYIMBO ZA IBADA

Tunazo Ibada nyingi katika Kanisa la Orthodoksi. Kila Ibada, ina nyimbo maalum zinazofaa kuimbwa. Liturghia Takatifu ni mojawapo ya Ibada hizi. Kuna aina nne za Liturghia: 1. Ya Mtakatifu Yohana Krisostomu (huadhimishwa mara nyingi mwakani). 2. Ya Mtakatifu Basilio Mkuu (huadhimishwa mara kumi mwakani). 3. Ya Mtakatifu Yakobo (huadhimishwa mara moja tu, tarehe 23 Oktoba – makumbusho yake) . 4. Liturghia ya Vipaji Vilivyotakasika (Wiki zote za Mfungo Mkuu. Siku ya Maria Kupashwa Habari Njema [Machi 25], Liturghia ya Mtk. Yohana Krisostomu huadhimishwa). Tunazo Ibada zingine kama Mazishi, Ndoa, Ubatizo…, na zingine nyingi.