August 13, 2026

Swahili Orthodox Chants & Teachings

Ili kwa nia moja tuungame: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Wimbo kwa Mzazi-Mungu

Katika Liturghia Takatifu, kunayo nafasi ya wimbo kwa Mzazi-Mungu ambao huwa unabadilika kulingana na muhula mwakani. Wimbo ujulikanao zaidi na ambao ni mfano mwema ni ‘Ni wajibu kweli kukuita heri’.