August 13, 2026

Swahili Orthodox Chants & Teachings

Ili kwa nia moja tuungame: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Hebu jiulize



Bwana Yesu alitamka:
“Mimi ndimi njia ya kweli,
mtu haji kwa Baba yangu
ila kwa njia yangu mimi.”

Hebu jiulize (jiulize);
njia gani uifuatayo?
nawe, waelekea wapi?
na, wafuata njia ya kweli?

Ngamia ni rahisi sana
kuingia tundu la sindano
kuliko mtu mwenye dhambi
kuingia ufalme wa mbinguni.

Mimi ni alpha na omega,
mimi ni mwanzo tena mwisho,
mtu haji kwa Baba yangu
ila kwa njia yangu mimi.

Njia nyembamba yenye shida
ndiyo iendayo mbinguni,
nayo pana yenye raha
yaelekea Jehanamu.

source