August 13, 2026

Swahili Orthodox Chants & Teachings

Ili kwa nia moja tuungame: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Masumbuko ya kimwili – Maisha ya Mtk. Yakobo wa Evia



Yakini haya: Sote twapita njia tu maishani haya, magonjwa mbalimbali na mateso yakiwa sehemu ya mafunzo yetu ndani ya upendo wa Mungu na katika kuwa washiriki wa Ufalme Wake wa Mbinguni. Akiwa ameshushwa kutoka Paradiso, alikokuwa amewekwa punde tu alipoumbwa na Mungu. Binadamu kwa njia moja au nyingine huyapitia mateso yasiyoepukika, lakini kwa jitihada za kuwa washindi dhidi ya dhiki zote, na kwa kufunzwa kanisani, huipekua njia yake ya kurudi paradisoni tena. Hicho ndicho kilichomtendekea Padre Yakobo. Hakukombolewa kutokana na maradhi yake ya kimwili lakini tatizo lake lilitatuliwa Kanisani, kupitia kwa Watakatifu Wake. Kwa sababu hii, hakuwa na wasiwasi wa kitakachomtendekea, kama ilivyodhihirika katika maisha yake ya utakatifu yaliyojawa na kusumbuka kwingi…..”

— Profesa Stiliano Papadopulo

Shamba la Roho Mtakatifu: Mtakatifu Yakobo wa Evia.

Tafsiri toka kwa: www.Orthodoxwitness.org/saint-Iakovos
Watafsiri: Swahili Orthodox Chants & Sammy Psalmist

source