August 13, 2026

Swahili Orthodox Chants & Teachings

Ili kwa nia moja tuungame: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Mtk Nikodemu – Kutunza Hisia Zetu



Sababu ya kila mmoja kung’ang’ana kuzitunza hisia zake.

Kulingana na Mtakatifu Giorgio Mtheolojia, lazima tung’ang’ane kudhibiti hisia zetu na kuzitunza, maana ndizo njia rahisi za kuelekea maovuni na za kuingia dhambini. Tujiepushe na njia hizi rahisi za kuelekea maovuni na za kuingia dhambini. Nasema kwenu basi, tieni juhudi zenu zote katika kutunza hisia zenu. Pia nawaambieni kwamba muwe makini, mng’ang’ane, na nasisitiza hili kwa kutumia visawe kadhaa. Nataka niwathibitishie kwamba shetani huwa amesimama mbele yetu kila wakati, akitazama na kusoma hali ya hisia zetu. Punde tu tufunguapo hisia hata moja kwake, huingia moja kwa moja nafsini mwetu na kutuletea kifo, kama vile adhihirishavyo Mtk. Isaka: “Adui amesimama na kututazama moja kwa moja machoni mchana na usiku ili kubaini ni njia ipi ya hisia zetu tutakayomfungulia aingie. Aingiapo kupitia mojawapo ya hisia zetu kwa kutokuwa waangalifu, hapo huyu mbwa mjanja asiyekuwa na haya hutushambulia zaidi kwa mishale yake mwenyewe.”

source