Hivyo basi utusiwapo na mtu, mfikirie kwa adhabu atakayoipata ; na hapo bali na kutokasirika, hata machozi utayalia kwa ajili yake.
Vilevile, hata kama unatamani ujilipishie, tulia kwa ajili ya amani yako mwenyewe, na kwa hiyo umempinga milele adui yako ; kama utamrushia matusi juu ya matusi yake, hapo umewasha moto. “Lakini”, mmoja asema, “watutazamao hutuita dhaifu tutuliapo ili kutunza amani.” Hapana, hawataulaumia udhaifu wenu, lakini watawatamani kwa hekima yenu. Kadhalika, uumizwapo na ujeuri, hufanyika jeuri ; uumizikapo, hulazimisha watu kufikiri kwamba kilichosemwa ni ukweli. Kwa sababu gani, niambie, mtu tajiri hucheka aitwapo maskini? Si kwa kuwa anafahamu yeye si maskini? Hivyo basi kama tutacheka tutusiwapo, tutaweza kutoa ithibati tosha kwamba hatuyajui madai tutuhumiwayo.
Hivyo acheni tukue kiroho, na hivyo kumdhibiti mnyama mwitu huyu atishaye. Hasira haitofautiani kamwe na wendawazimu, ni shetani wa muda, au tuseme ni kitu kibaya hata zaidi ya kuwepo kwa shetani; maana aliye na shetani aweza samehewa, lakini mtu mwenye hasira apaswa adhabu elfu kumi, kwa hiari hujiingiza kwenye shimo la uharibifu na kabla ya jehanamu huja adhabu ya mateso tayari kutokana na hili, kwa kuleta machafuko fulani na mawimbi ya hasira zisizotulizika, usiku kucha na mchana wote, kwa mawazo ya nafsi yake. Hivyo basi, ili kujiepusha kutokana na adhabu hapa na kisasi baadaye tutokapo hapa, tuitupilie hii tamaa baya na badala yake tuonyeshane upole na utulivu, ili tupate pumziko la nafsi zetu hapa na katika Ufalme wa Mbinguni. Na tujaliwe sisi sote, kwa neema na rehema za Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kupitia kwake na pamoja naye, kwa Baba na Roho Mtakatifu uwe utukufu, sasa na siku zote na ulimwengu bila mwisho. Amina.
source
Recent posts
Apolitikio ya Pentekoste
Hebu jiulize
Apolitikio ya Kuzaliwa kwa Kristo (Live class with Nyandarua Youths)