Hymns for Sunday 15th March 2020 Lyrics
Resurrectional Apolytikion, Tone 6
Angelic powers were in Your sepulchre,/ and those who guarded You became as men long dead;/ and standing there was Mary by Your tomb seeking / Your pure and sacred body,/ You despoiled hades; yet tempted not by him was You,/ You did meet the Virgin O life bestower./ O You who rose from the dead,/ glory to You O Lord.
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
Apolitikio ya Mt. Grigori Mtenda-miujiza (Grigori Palama) – sauti ya nane (8)
Mwanga wa imani ya Kiothodoksi,/ mwamba imara / wa Kanisa na mwalimu wake,/ aliyejuzwa na Mungu,/ wewe ni pambo la watawa,/ jemadari asiyeshindwa wa wanatheolojia,/ Ee Grigori Mtenda-miujiza,/ na pendo la Thessaloniki,/ malaika wa neema,/ usikome milele kuomba kwa ajili,/ ya wokovu wa roho zetu.
Sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina.
Theotokio ya ufufuo – sauti ya 8
Ee Mwema uliyezaliwa / na Bikira / kwa ajili yetu, na kuvumilia / mateso ya Msalaba / na ukanyakua / mauti kwa mauti, / na kuonyesha / kuonyesha* / ufufuo kwa sababu U Mungu. / Usiwaache hao / ambao / uliwaumba kwa Mkono Wako. / Ee Mwenye rehema, / uonyeshe / upendo Wako kwa wanadamu, / na kumpokea Mzazi-Mungu/ aliyekuzaa / anayetuombea Kwako. /. Na uwaokoe ambao // hawana kimbilio, Ee Mwokozi wetu.
Anavathmi – Sauti ya 6 (2nd Plagal/sauti 2b)
Nimekuinulia macho yangu / wewe uliye Mbinguni;/ nirehemu,/ ili niishi katika Wewe.
Utuhurumie sisi watupu,/ na ututayarishe kuwa vyungu vya kutumika.
Utukufu kwa Baba,/ na Mwana na Roho Mtakatifu.// Sasa na siku zote,/ hata milele na milele. Amina.
Katika Roho Mtakatifu / ni kusudi ya kuokoa vyote;/ akiwa anampulizia kadiri yake mtu,/ anamtoa katika vitu vya nchi,/ kumpa mabawa,/ na kumkuza na kumweka juu.
Prokimeno
Ee Bwana inua nguvu Yako,/ na uje kwa ajili ya wokovu wetu. X2
Mstari: Sikiliza, ewe mchungaji wa Israeli.
Ee Bwana inua nguvu Yako,/ na uje kwa ajili ya wokovu wetu.
Alleluia baada ya kusoma waraka – sauti ya sita (2nd Plagal/Sauti 2b)
Alleluia Alleluia Alleluia
Mstari: Aketiye mahali pa siri pa aliye juu, atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
Alleluia Alleluia Alleluia
Mstari: Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu.
Alleluia Alleluia Alleluia
source
Recent posts
Apolitikio ya Pentekoste
Hebu jiulize
Apolitikio ya Kuzaliwa kwa Kristo (Live class with Nyandarua Youths)