Hymns for Sunday 29th March 2020
Apolitikio ya Ufufuo Sauti 8
Ulishuka mbinguni Ee mwenye huruma/ ukawa kaburini muda wa siku tatu;/
Ili tuwe huru,/ mbali na tamaa mbaya,/
Uzima na ufufuo wetu,/ Ee Bwana,
Utukufu Kwako.
Utukufu kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
Apolitikio ya Mt. Yohana (Climacus) – Sauti 8
Kwa wingi wa machozi yako/ ulifanya nyika kavu kuotesha;/ na kwa ishara za undani mwako,/ ‘kafanya juhudi zako kuzaa matunda mara mia;// na ukawa nyota, ukiangazia uli•mwengu kwa miujiza yako,// Ee Yohana, baba yetu mtawa.// Tuombee kwa Kristo Mungu wetu,// kwa ajili ya wo•kovu wa roho zetu.
Sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina
Theotokio ya ufufuo – sauti 8
Ee Mwema uliyezaliwa / na Bikira / kwa ajili yetu, na kuvumilia / mateso ya Msalaba / na ukanyakua / mauti kwa mauti, / na kuonyesha / kuonyesha* / ufufuo kwa sababu U Mungu. / Usiwaache hao / ambao / uliwaumba kwa Mkono Wako. / Ee Mwenye rehema, / uonyeshe / upendo Wako kwa wanadamu, / na kumpokea Mzazi-Mungu/ aliyekuzaa / anayetuombea Kwako. /. Na uwaokoe ambao / hawana kimbilio, Ee Mwokozi wetu.
source
Recent posts
Apolitikio ya Pentekoste
Hebu jiulize
Apolitikio ya Kuzaliwa kwa Kristo (Live class with Nyandarua Youths)