IDIOMELA
Mstari: Ee Mungu unirehemu, sawasawa na fadhili Zako; kiasi cha wingi wa rehema Zako, uyafute makosa yangu.
Ee Mwema uliyeitakasa dunia nzima kwa mwanga Wako, uligeukia mahali pa mlima ulio juu; na kwa wanafunzi Wako ulionyeshana nguvu Yako, kuwa waikomboa dunia toka dhambini. Hivyo basi twakulilia: Ee Bwana wa rehema, ziokoe nafsi zetu!
ANTIFONA YA PILI
Ee Mwana wa Mungu, uliyegeukia Mlimani Tabori, utuokoe. Twakuimbia, Alleluia.
WIMBO WA INGILIO DOGO • Sauti 2
Maana Nawe, Bwana, ni chemichemi ya uzima; mwangani Mwako tutauona mwanga. Ee Mwana wa Mungu, uliyegeukia Mlimani Tabori, utuokoe. Twakuimbia, Alleluia.
WIMBO WA USHIRIKA
Tutatembea mwangani mwa utukufu wa uso Wako, Ee Bwana, milele. Alleluia.
source
Recent posts
Apolitikio ya Pentekoste
Hebu jiulize
Apolitikio ya Kuzaliwa kwa Kristo (Live class with Nyandarua Youths)