August 13, 2026

Swahili Orthodox Chants & Teachings

Ili kwa nia moja tuungame: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Swahili antiphons of the Transfiguration (Aug 6)



#Mistari_Kamili_Ya_Antifoni_Hapa:

ANTIFONI I
1. Bwana ndiye aliye mkuu, na mwenye kusifiwa sana; katika mji wa Mungu wetu.

Kwa maombi ya Mzazi Mungu, Ee Mwokozi, utuokoe.

2. Milima waiweka imara kwa nguvu Zako.

3. Umejivika nuru kama vazi.

4. Milima itajawa na furaha, katika uwepo wa Bwana.

ANTIFONI II
1. Misingi Yake ipo juu ya milima mitakatifu.

Ee Mwana wa Mungu, uliyegeukia mlimani Tabori, utuokoe sisi twakuimbia, Alleluia.

2. Bwana ayapenda malango ya Sayuni kuliko maskani zote za Yakobo.

3. Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee mji wa Bwana.

4. Mwanadamu atasema, “Mama Sayuni,” na mwanadamu kazaliwa toka kwake.

source