Ee Bwana wahimidiwa nifundishe amri Zako.
Jamii ya watakatifu imeona chemichemi ya uzima na lango la paradiso, niweze Nami kuiona njia kwa kutubu; mimi ndimi kondoo aliyepotea, nirejeshe Ee Mwokozi na uniokoe.
Ee Bwana wahimidiwa nifundishe amri Zako.
Ewe uliyeniumba kutoka bure na kwa mfano Wako mtakatifu ‘kanipa heshima; lakini, kwa kuasi amri Zako, ulinirudisha udongoni mahali nilitolewa. Niongoze unirudishe niumbwe tena kwa uzuri wa kale wa sura Yako.
Ee Bwana wahimidiwa nifundishe amri Zako.
Mimi ndimi mfano wa utukufu Wako usionenwa, ingawa nina makovu ya kuanguka kwangu; unirehemu mimi kazi ya mikono Yako, Ee Bwana mweza. Na unisafishe kwa fadhili Zako, na unihifadhie makao yatamaniwayo na moyo wangu, kwa kunifanya mwana wa paradiso.
Ee Bwana wahimidiwa nifundishe amri Zako.
Pumzisha Ee Mungu, roho za watumishi Wako; na uwateulie mahali katika paradiso, ambapo jamii za watakatifu na wenye haki watang’aa kama nyota. Kwa watumishi Wako walalao sasa pumzisha, ukitupilia mbali makosa yao yote.
Utukufu kwa Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.
Nuru ya Utatu ya Mungu mmoja kwa sauti ya nyimbo za usujudu na tulie; Mtakatifu ni wewe Baba wa milele, na Mwana pia wa milele na Roho Mtakatifu. Tuangazie mwanga Wako tukuabuduo kwa imani, na toka kwa moto wa milele utuokoe.
Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Salamu Bibi wa neema umzaaye mwilini Mungu kwa wokovu wa wote. Kupitia Kwako binadamu amepata wokovu, Kupitia Kwako tupate kuiona paradiso; Mzazi Mungu, bibi wetu bila doa na mbarikiwa.
Alleluia Alleluia Alleluia, utukufu Kwako Ee Mungu wetu. X3
source
Recent posts
Apolitikio ya Pentekoste
Hebu jiulize
Apolitikio ya Kuzaliwa kwa Kristo (Live class with Nyandarua Youths)