August 13, 2026

Swahili Orthodox Chants & Teachings

Ili kwa nia moja tuungame: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; Utatu wa asili moja, na asiyetengana.

Swahili Idiomela of the Departed, 5th tone



#OrthodoxFuneral #Idiomela #fifthmode

Nakumbuka mawazoni nabii aliyesema; “Mie ni udongo tena vumbi”. Mara tena, kwa makini nikaangalia kaburini na kuiona mifupa humo, kavu bila nyama. Na nikasema; “kweli, ni nani mfalme na ni nani askari, nani tajiri nani maskini, nani mwenye haki nani mwenye dhambi?”. Lakini, kwa watumishi Wako, Bwana; pamoja na watakatifu, pumzisha.

I Called to mind the Prophet who shouted, “I am but earth and ash.” And once again I looked with attention on the tombs, and I saw the bones therein which of flesh were naked; and I said, “Which indeed is he that is king? Or which is soldier? Which is the wealthy, which the needy? Which the righteous, or which the sinner?” But to Your servant, O Lord, grant that with the righteous he (she) may repose.

source