#OrthodoxFuneral #Trisagion #MemorialService
Pamoja na roho za wenye haki waliostahilishwa katika imani, pumzisha Ee Bwana, roho za watumishi Wako. Na uzihifadhi uzimani ulio mbarikiwa, wa kuishiwa Nawe, Ee mpenda wanadamu.
Mapumzikoni Mwako, Ee Bwana, walalamo watakatifu Wako wote; pumzisha pia roho za watumishi Wako, maana Wewe ndiwe pekee usiyekufa.
Utukufu kwa Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.
Wewe U Mungu wetu uliyeshuka kuzimuni, kulegeza machungu ya wafu walio humo. Pumzisha pia roho za watumishi Wako, Ee Mwokozi.
Sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina.
Ee Bikira pekee mtakatifu na bila doa, uzaoni mwa ubikira ulimleta Mungu. Ombea roho za watumishi Wako ziokolewe.
source
Recent posts
Apolitikio ya Pentekoste
Hebu jiulize
Apolitikio ya Kuzaliwa kwa Kristo (Live class with Nyandarua Youths)