Sauti 7
Enyi Mashahidi watakatifu, ninyi mfano na matendo yenu yamejishindia taji la utukufu, tuteteeni kwa Bwana wetu, na kumwomba huruma Zake kwa nafsi zetu hata milele.
Utukufu kwa Kristo Mungu wetu, taji la Mitume wote, kwa furaha Mashahidi walitangaza kwamba Utatu ni mmoja kiasili hata milele.
Sauti 5
Shangilia Isaya, kwani Bikira katunga mimba, na kumzaa Mwana ambaye aitwa Imanueli, aliye Mungu na binadamu, macheleo ni jina Lake, tukimtukuza twaita Bikira mbarikiwa.
source
Recent posts
Apolitikio ya Pentekoste
Hebu jiulize
Apolitikio ya Kuzaliwa kwa Kristo (Live class with Nyandarua Youths)