Orthodox Patriarchal Ecclesiastical School Nairobi Choir
1. Vizazi vyote, vinaleta wimbo; kwa mazishi yako Kristo wangu
2. Alipokutoa kwa mti, Arimateos alikuzika; katika kaburi.
3. Wabebaji wa mafuta; walikuletea manemane, mapema na akili Kristo wangu
4. Wee Jira langu tamu; mwana wangu mpendwa, ubora wako ulichwea wapi?
5. Wabebaji wa mafuta; walinyunyizia manemane, kaburi yako walipofika mapema.
6. Kanisani amani; na watu wako wokovu, peana katika kufufuka kwako
7. Mwili mpaji wa uhai; Yosefu anauzika, pamoja na Nikodemu
8. Wee Mwanga wa macho yangu, mwana wangu mpendwa, umejifichaje kaburini
9. Mtumwa mpumbavu; mtume mwanzilishi, alisaliti hekima ya milele
10. Yuda Yule mlagai; alimuuza mkombozi, alijikuta mwenyewe mfungwa
11. Yosefu; na Nikodemu, walikuzika kaburini
12. Ee mwanga wa macho yangu; mwana wangu mpendwa, umejifichaje kaburini?
13. Mama yako asiye na doa; aliomboleza, wee Neno ulipokufa
14. Mlagai alindanganyika; na Yule aliyendanganywa, amekombolewa kwa hekima yako
15. Ee mwana wa Mungu, mfalme wa wote Mungu wangu, na Muumba ulivumiliaje mateso?
16. Mama alilia kwa sauti; alipomuona mwanawe, akining’inia msalabani
17. Mtumwa alikuchoma moyo; kukuona ukiomboleza, na kutokwa na machozi
18. Ee mwanga wa macho yangu; ubora wa mwana, umejifichaje kaburini?
19. Inuka Ee mwenye huruma; na utuinue nasi, kutoka shimo la kuzimu.
20. Mama yako aliyekuzaa; alilia kwa machozi, “ inuka Ee mpaji wa uhai.”
21. Nguvu za mbinguni; zilishangaa kwa hofu, kukutazama ukiwa umekufa.
22. Yosefu alitoroka nawe; kwa uzee Ee Mwokozi, na sasa Yosefu mwingine anakuzika
23. Mama yako asiye na doa; alilia na kuomboleza, Ee Mwokozi wangu ulipouawa
24. Mawazo yalifunikwa; kwa kuzikwa kwa ajabu, na hofu yako Muumba wa wote
25. (Wabebaji wa manukato; walikuja mapema, na kunyunyiza kaburi manukato)x3
26. Kwa kufufuka kwako; kidhi amani kwa kanisa, na wokovu watu wote
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu
Wee utatu Mungu Baba; na Roho Mtakatifu, hurumia ulimwengu
Sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina
Wee Bikira wezesha, watumishi wako kuona, kufufuka kwa mwana wako.
Vizazi vyote, vinaleta wimbo; kwa mazishi yako Kristo wangu.
source
Recent posts
Apolitikio ya Pentekoste
Hebu jiulize
Apolitikio ya Kuzaliwa kwa Kristo (Live class with Nyandarua Youths)